Nay Wa Mitego ajifilisi, sasa arudi kutembelea bajaji

Tuesday October 10 2017

 

By FRANK NGOBILE


Kumekuwa na taarifa mbalimbali zikiendelea kusambaa juu ya Nay Wa Mitego kufulia mpaka kufikia hatua ya kuuza magari yake yote na sasa ameonekana mara kadhaa akitembea na bajaji hali ambayo haikuwa kawaida yake.
Akizungumza hilo Nay Wa Mitego alisema ni kweli ameamua kuuza magari yake yote ila kwa sababu anazojua yeye na si kama watu wengi wanavyosema.
“Kila mtu anazungumza lake ujue, lakini kama kuuza nimeuza kwa sababu zangu za msingi, nimemua kuachana na magari nipande daladala na bajaji, na hayo ndio maisha ambayo nimekulia, unajua mimi nimezaliwa kwenye maisha ya kawaida na mtaa ndio umenilea, kwa hiyo watu wasichoke kunipa lifti wakiniona, au wasishangae siku wakiniona natembea kwa mguu,” alisema.