Nandy wa kimataifa nyie

Muktasari:

  • Nandy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Afrimma katika kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki, alisema anawakubali nyota hao wawili vilivyo.

DIVA wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy ametamani kuanza kupaa anga kwa anga ili kufanya kolabo na nyota wa nje kama Yemi Alade na Wizkid kutoka Nigeria.

Nandy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Afrimma katika kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki, alisema anawakubali nyota hao wawili vilivyo.

“Napenda kufika mbali zaidi, muziki wetu sasa unatubeba, unachezwa sehemu nyingi. Kwa upande wa kolabo ninatamani zaidi kufanya kazi na Yemi Alade na Wizkid, wako vizuri,” alisema.

Mwanadada huyo anayetamba na kibao cha Mahabuba akishirikiana na Aslay, aliliambia Mwanaspoti kuwa katika kinyan’ganyiro cha kuwania tuzo hizo za Afrimma alikuwa anawahofia Vannesa Mdee na Feza Kessy ambao nao ni moto.

“Kwanza niwashukuru watanzania kwa kuniwezesha kutwaa hii tuzo, pili katika kinyan’ganyiro hiki, niseme tu ukweli nilikuwa nawahofia Vannesa Mdee na Feza Kessy,” alisema.