Nandy bana, kumbe naye yumo

Muktasari:

  • Nandy alisema kabla ya kushika namba hiyo, ilikuwa ikishirikiliwa na Lady Jaydee, ambaye anaendelea kumheshimu kwa kuwa amemtangulia katika fani.

MSANII wa Bongofleva, Nandy amesema yeye ni msanii wa kike namba moja Tanzania.

Nandy alisema kabla ya kushika namba hiyo, ilikuwa ikishirikiliwa na Lady Jaydee, ambaye anaendelea kumheshimu kwa kuwa amemtangulia katika fani.

“Ukiniuliza kuhusu msanii bora wa kike, namba moja lazima nitajitaja miye, japo zamani namba moja yangu alikuwa Lady Jaydee,na nitaendelea kumheshimu siku zote kwa kuwa amenitangulia kimuziki,”alifunguka Nandy

Hata alipoulizwa kati ya Vanessa Mdee, Ruby na yeye nani namba moja, Nandy hakutaka kujiweka nyuma alisema atakuwa yeye tu kutokana na kujiamini na uwezo wake wa kuimba.