Nameless atoboa kilichomuweka kwa miaka 20

Muktasari:

Katika kipindi alichofanya muziki wamekuja wasanii wengi, wakatisha na kisha kupotea lakini yeye amesalia kuhangaisha.

STAA mkongwe wa burudani, Nameless amefichua siri tatu ambazo amesema zimemwezesha kudumu kwenye gemu kwa zaidi ya miongo miwili bila ya kupotea wala kutetereshwa na ushindani mpya wa kimuziki hasa kutoka kwa wasanii chipukizi.
Katika kipindi alichofanya muziki wamekuja wasanii wengi, wakatisha na kisha kupotea lakini yeye amesalia kuhangaisha.
Akifunguka, Nameless amesema kwa msanii chipukizi anayetamani kubakia staa kwa miaka mingi  pasi na kupotea basi atahitaji kukopi vitu vitatu alivyozingatia yeye ili kumfikisha alipo kwa sasa.
“Kwa wasanii wachanga waelewe kuna talanta, halafu kuna nidhamu na cha tatu ni kuwa na mipango. kuna watu wana talanta ila wanakosa nidhamu huyo hatafika mbali. Wengine wana talanta na nidhamu ila hawana mipango, huyo hawezi kutisha kwa muda mrefu. Lazima vitu hivi vitatu viendane hakuna ujanja. Msanii lazima ajitahidi kuhakikisha ana sifa hizo ndipo atadumu kwenye gemu kwa muda mrefu,” Nameless akatoa darasa.