Dogo Janja anusurika kwenda jela

Wednesday November 8 2017

 

By RHOBI CHACHA

Mwamuziki wa muziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ameibuka na kusema kuwa, kabla ya kutokuwa maarufu alikuwa ni muhuni, mtukutu na mwenye kiburi.

Dogo Janja amesema, kwa dunia hii ya sasa angekuwa jela au hata marehemu kwani wenzake wengine wamepigwa mawe mpaka kufa kwa sababu ya utukutu, unyang’anyi na matukio kama hayo.

Aidha ameongeza kuwa, amejifunza kitu kutokana na makosa ndio maana ameamua kubadilika na kuachana na hizo tabia.