Msanii Avril wa Kenya ambwatukia AT

Friday July 21 2017

 

Msanii Avril Nyambura amemtolea uvivu, nguli wa ngoma za mduara kutoka Tanzania, AT kwa kusema hana muda mchafu wa kujibizana naye, ikiwa ni baada yake kudai kuwa mrembo huyo hajui kuimba.

“Nimeshawahi kwenda Ogopa Deejays kufanya nyimbo na Avril na kwa sababu aliimba utumbo mimi nilimtoa” alidai AT kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni na redio moja jijini Dar es Salaam.

Avril alisema, “Halafu namshangaa mbona imemchukua miaka yote hii ndio aje kuropoka. Huyo haelewi anachokizungumizia ajiangalie upya.”

 Avril aliyeondoka Ogopa Records 2012  na kwa sasa yupo kwenye msimu wa sita wa Coke Studio unaoendelea kurekodia hapa jijini Nairobi.