Moze Iyobo atangaza ndoa na Aunty Ezekiel

Monday May 14 2018

 

By Nasra Abdallah

Dansa wa msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul' Diamond', Moze Iyobo ametaja siku ambayo anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Aunty Ezekiel.

Akizungumza na MCL Digital, Moze ambaye ni baba wa Cookie, mtoto aliyempata kwa Aunty miaka mitatu iliyopita amesema siku ambayo atafunga ndoa na mchumba wake huyo ni pale atakapomuongezea mtoto wa pili.

"Sasa hivi siwezi kutaja tarehe hasa lini tutafunga ndoa na mzazi mwenzangu, kwani nasubiri hadi apate mtoto wa pili yaani mdogo wake Cookie, hapo ndipo nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza,"amesema Iyobo.

Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa filamu ya Mama ni Mungu wa Dunia, dansa huyo amekiri  kuwa na mchango mkubwa katika utengenezaji wake ambapo Aunty na Cookie wamecheza kama wahusika wakuu.