Mkwanja wa Ali Kiba kila shoo sio mchezo

Muktasari:

  • Kila kampuni hutaka kufanya kazi na wote hao na Safaricom imekuwa wateja wao wakubwa.

Kabla ya kuchipuka kwa Diamond, Kiba ndiye aliyekuwa msanii maarufu zaidi wa Bongo Flava. Sasa hivi wawili hao wanashindania biashara. Wameunda brandi kubwa na kuzifanya kampuni nyingi kuwa zikiwapigania.

Kila kampuni hutaka kufanya kazi na wote hao na Safaricom imekuwa wateja wao wakubwa.

Staili yake Ali ya fasheni na mtindo wake wa muziki umechangia kumtofautisha kabisa na wasanii wengine.

Pia, naye anavuta dili za kimatangazo kwao Tanzania. Kwa upande wa malipo, aliwahi kukiri kuwa hulipwa Tsh8 milioni kwa shoo za nyumbani.

Akiwa nje ya Tanzania hasa anapopiga shoo  Kenya, yeye hutoza kati ya Sh2 milioni hadi Sh5, milioni kwa kutegemea na kazi.