Meghan ageuziwa kibao mapemaa

Muktasari:

  • Mgogoro huo umekuja kufuatia kile kinachodaiwa kuwa hamjali baba yake.

MIEZI michache baada ya kufunga ndoa na mwana mfalme Prince Harry, Meghan Markle amejikuta kwenye mgogoro mkubwa na familia yake.

Mgogoro huo umekuja kufuatia kile kinachodaiwa kuwa hamjali baba yake.

Dada yake Meghan, Samantha Markle amefikia hatua ya kumshambulia ndugu yake hadharani na kudai endapo baba yao atakufa lawama zitakuwa kwake.

Samantha ametoa povu hilo na kudai anashangazwa na ndugu yake anavyowaenzi na kuwajali watu wengine wakati hana muda na baba yake.

“Kwanini usimuenzi baba yako imetosha sasa, kuwa binadamu, kuwa kama mwanamke. Baba yetu akifariki lawama zote ni kwako Meg,”

“Unatoa heshima kwa watu wengine na kumdharau baba yako hayo ni maajabu,” aliandika Samantha kwenye ukurasa wake wa Twitter.