Manfongo aipa shavu Mwanaspoti

Muktasari:

Shoo hiyo ilifanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhem.

MKALI wa nyimbo za singeli, Manfongo, amewataka wasomaji wa magazeti nchini kuchangamkia promosheni ya ‘Zali la Mwanaspoti’ inayoendeshwa na gazeti hili ili wabadilishe maisha yao.

Manfongo anayetamba na vibao vyake vya ‘Hainaga Ushemeji’ na ‘Sio Poa’ alitoa kauli hiyo wikiendi iliyopita wakati wa shoo ya kutoa elimu kwa wasomaji wa gazeti hili juu ya namna ya kushiriki promosheni hiyo ambayo kila wiki itatoa mshindi mmoja wa tiketi ya kwenda kutazama mechi ya Ligi Kuu ya England. Shoo hiyo ilifanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhem.

“Nalipongeza gazeti la Mwanaspoti kwa kuja na kitu hiki, wasomaji wanatakiwa kuchangamkia fursa hii kwani kwenda Uingereza sio jambo dogo,” alisema.

“Yaani ukinunua Mwanaspoti unapiga ndege wawili kwa jiwe moja. Utapata habari kemkem zikiwemo zetu akina Manfongo, pia una uhakika wa kujishindia zawadi kibao.”