Mama Njaidi kala shavu kiulainiii

Tuesday March 13 2018

 

MKONGWE wa filamu nchini, Hidaya Njaidi ‘Mama Njaidi’ amedai hana budi kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake kwa Wilaya ya Ubungo kutokana na harakati zake za shughuli za kijamii.

Mama Njaidi akawashtua wenzake kwa kuwataka wajitoe mbele ya jamii hasa kwa kuwasaidia watu wenye shida katika maeneo waishiyo ili wajitengenezee heshima.

“Najitaidi kufanya kazi nguvu sana ili kuweza kuwasaidia wenye shida naigiza nafanya ujasiriamali na kuwahamasisha wasanii wenzangu kuwasaidia wengine kama ninavyofanya mimi kuwasaidia watoto wa mgongo wazi,” alisema.

Mama Njaidi alisema kuwa, kuna watu huguswa na filamu zao wakiangalia maisha waishio jamii na kuwakilisha katika filamu, hivyo wengi wana imani na wasanii wa filamu kama wasanii wote watakuwa pamoja na kufikiria kuwa na kikundi cha kuisaidia jami itafanikiwa kwani watu wana imani na waigizaji.