Sanchi akimbiza wanaume aisee

Muktasari:

Sanchi, ambaye amekuwa gumzo kwelikweli kutokana na umbo lake la kuvutia, amesema kama kuna ma Mrembo aliyejipatia umaarufu kwa sasa amekuwa akiogopwa na wanaume kutokana na dau lake la mahari.

KAMA una hela zako za mawazo basi usipoteze muda wako kabisa kumwazia mrembo anayetikisa kwenye mitandao ya kijamii, Sanchi.
Sanchi, ambaye amekuwa gumzo kwelikweli kutokana na umbo lake la kuvutia, amesema kama kuna ma Mrembo aliyejipatia umaarufu kwa sasa amekuwa akiogopwa na wanaume kutokana na dau lake la mahari.
Hivi karibuni mrembo huyo aliweka bayana kwamba, kama kuna mwanaume anataka kumuoa basi ajipange kwelikweli kwa kuwa, mahari yake sio chini ya sh 20 milioni.
“Wanaume wanaogopa kutangaza ndoa sababu ya dau la mahari yangu. Wanaokuja ni wale ambao hawana nia ya kuoa, ambao kwa sasa siwahitaji kabisa,” alisema Sanchi.