Kwa Wastara mambo ni moto, lazima kieleweke

Muktasari:

“Ningeomba wasanii na wadau wengine tumchangie msanii mwezetu kwa ajili kupata matibabu ya mguu wake, kwa kweli anaumwa kila mmoja wetu akitoa kile alichonacho kitamuondolea maumivu Wastara,” alisema Dk. Mwakyembe.

LA Mgambo limepigwa na lazima suala la Wastara likae sawa. Unajua kwanini? Waziri wenye dhamana ya michezo na sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe ameamua kuingilia kati ishu ya msanii huyo na kuwaomba wenzake na wadau wa filamu kumpiga tafu ili apate matibabu ya maradhi yanayomsumbua.

“Ningeomba wasanii na wadau wengine tumchangie msanii mwezetu kwa ajili kupata matibabu ya mguu wake, kwa kweli anaumwa kila mmoja wetu akitoa kile alichonacho kitamuondolea maumivu Wastara,” alisema Dk. Mwakyembe.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo na kufika pia nyumbani kwa Wastara, Tabata Sanene, Dar es Salaam ili kumjulia hali akiongozana na Katibu Mtendeji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mwingireza.

Dk. Mwakyembe alimchangia Wastara kiasi cha Sh 1 milioni ikiwa ni hamasa kwa wadau wengine wakiwamo wasanii kumpiga mwanadada huyo.