Kumpenda asiyekupenda ni ujinga ndugu yangu

Muktasari:

  • Kuna mambo ambayo kama utayaendekeza au unayaendekeza, utakuwa unakosea sana na kama hutajali, utajikuta unalia kila siku kwa sababu ya mapenzi hasa kumpenda mtu asiyekupenda.

Hili ni swali ambalo litakuwa linakutesa sana akilini. Kwa nini napenda hivi? Ana nini? Kwa nini sio mwingine? Hata hivyo, pamoja na kujiuliza maswali hayo, bado wewe unaendelea tu kuumia na kuacha hali hiyo kuwa kama ilivyo.

Ngugu yangu, acha kujidanganya, kama mtu umempenda na yeye hakupendi inaonyesha wazi, hakuna kificho. Acha kujidanganya kuwa ipo siku atabadilika.

Kuna mambo ambayo kama utayaendekeza au unayaendekeza, utakuwa unakosea sana na kama hutajali, utajikuta unalia kila siku kwa sababu ya mapenzi hasa kumpenda mtu asiyekupenda.

UTAKUA MTUMWA WA MAPENZI

Sawa, una mtu wako unampenda na ukadhani kwamba naye anakupenda. Ila ndugu yangu, kama kupenda kupo kupo tu, hata siku moja usijidanganye kupenda sana ndo kudumisha uhusiano, penda tu kawaida na kila mmoja ataelewa kwa sababu mpo pamoja.

Mambo ya kuenda hadi ukakosa raha, sio vizuri. Kwa nini ukose raha wakati mwenzako hata hajali kama unakosa hiyo raha na amani.

kwa nini ujiweke kwenye wakati mgumu kuwaza mtu ambaye anachukuliaa uhusiano wenu kawaida tu japo anakupenda, wewe ndo kuwa na kiherehere cha kupenda kupitiliza. Hapo unakosea ndugu.

Usifikie zaidi yake hakuna mwingine, eti kama utaachwa au mtaachana ndio basi hutapata mwingine ndio maana uwe mtumwa wa penzi. Unakosea sana.

HATAKUJALI

Katika ulimwengu wa mapenzi, ukiwa miongoni mwa wapenzi wanaopenda bila kupendwa ujue utateseka siku zote za maisha yako, kwani mpenzi wako hawezi kukujali, utakuwa na kazi ya kuhakikisha unamjali wewe. Hilo ni tatizo kubwa sana katika ulimwengu wa mahaba.

Utamtumikia kwa asilimia mia, hatakutimikia kwa lolote zaidi mshahara wa kukutesa siku zote zinazoitwa leo.

Utakuwa na kazi ya kumpigia simu, na kutaka kujua habari zake, ingawa hutaona akikukumbuka wala kukupigia simu, na endapo atafanya hivyo basi atakupigia akiwa na shida muhimu kutoka kwako.

Ukianza kuegemea kwenye penzi la utumwa huwezi kujielewa unateseka, watu ndio wataanza kukuonea huruma bila wewe kujali.

Watu wa karibu yako wataona mwili wako unakwisha na kubaki mifupa mitupu.

Utajijua ulipotea baada ya kushauriwa uachane naye anayekutesa na utakapopata mwingine anayekupenda na wewe kumpenda, yaani mkapendana sana ndipo utaona kweli ulikuwa ulimwengu wa giza na mateso.

SIO SEHEMU SAHIHI KWAKO

Mtu anapokupenda, kwanza atakujali kwa kila kitu, atakuonea huruma na kupenda kuona ukiwa na furaha siku zote za maisha yako. Ni mtu mnyenyekevu kwako, anayetaka kukupenda kila sekunde ya pumzi zako.

Hivyo hata kama hana kitu, nawe unashida na jambo atahangaika na kukukikisha anakutuliza roho yako, na sio kukuumiza.

Lakini madhara ya kumpenda mtu asiyekupenda hawezi kuwa sehemu ya mwili wako, yaani ukiumia atafurahia na kukuona mjinga.

La msingi ni wewe tu kuamua moja, haina haja ya kuwa sehemu utakayoishi kitumwa na kukosa amani na raha kwenye nafsi yako kisa tu ulimpenda. Ni bora ukawahi kufungua ukurasa mpya wa maisha yako ya uhusiano.