Kumbe Brad Pitt humwambii kitu kwenye pombe

Muktasari:

Hata hivyo, Pitt alikanusha madai kuwa hali hiyo imemsababishia aingie kwenye ulevi uliopitiliza ili kutuliza mawazo.

KWA mara ya kwanza mwigizaji wa Hollywood, Brad Pitt amekiri kuwa kuvunjika kwa ndoa yake kulimvuruga kichwa na kumweka mahali pabaya.

Hata hivyo, Pitt alikanusha madai kuwa hali hiyo imemsababishia aingie kwenye ulevi uliopitiliza ili kutuliza mawazo.

Katika mahojiano aliyofanya na GO Style, Pitt alisema pombe haina uhusiano wowote na ndoa yake kwani, siku zote tangu ujana wake amekuwa akitumia kilevi hicho.

“Sikumbuki hata siku moja niliyowahi kulala bila kupata kilevi, napenda sana mvinyo kwa hiyo hakuna ukweli wowote kwamba, nimeingia kwenye ulevi kwa ajili masuala ya talaka,” alisema.