Kiki za kulazimisha zinaua muziki Bongo

Muktasari:

Katika mahojiano na mwandishi Pancho anasema muziki wa sasa umejaa kiki sana tofauti na kuthamini vipaji.

Mtayarishaji nguli kutoka studio kali za B Hits, Pancho Latino  amefunguka kuwa kwa sasa muziki unaelekea kufa na si kupanda kama wengi wanavyoona.
Katika mahojiano na mwandishi Pancho anasema muziki wa sasa umejaa kiki sana tofauti na kuthamini vipaji.
“Kiki kwa sasa ndio zinasukuma muziki. Bila kiki au kuwa na hela basi kwa sasa sahau kuhusu muziki na kwa namna hiyo vipaji vingi tunakosa na mwisho muziki kufa ndio maana nasema muziki unaelekea kufa kabisa,” alisema.
Pia mtayarishaji huyo hakuacha kusema kwa namna ambavyo anamkubali produza mwenzie, Luffa ambae anafanya kazi katika studio za Wanene na kumpa ushauri kuwa asikubali kutumika na wasanii wa Bongo.