Kajala aja kivingine, hataki shobo

Muktasari:

  • Staa huyo mwenye mvuto alisema katika kujihakikishia anaepukana na skendo zisizo na msingi ameamua kuwakwepa marafiki wambea na wanaopenda kusambaza maneno yenye chokochoko.

STAA wa filamu za Kibongo Kajala Masanja amesema amebadili mustakabali wa maisha yake na kujiamini kwake ndio sababu ya kuheshimika mbele ya jamii.

Staa huyo mwenye mvuto alisema katika kujihakikishia anaepukana na skendo zisizo na msingi ameamua kuwakwepa marafiki wambea na wanaopenda kusambaza maneno yenye chokochoko.

Kajala ameongeza hakuna skendo iliyomuumiza katika maisha yake kama ile ya kusingiziwa kuempora Wema Sepetu bwana.

“Kwa sasa nimeamua kuishi hivi, mambo yangu kimyakimya sababu sitaki skendo za ajabu zinazoshusha heshima yangu katika jamii,” alisema Kajala.