Jux wa Vanessa akerwa na skendo

Muktasari:

  • Jux ambaye anashea vya ndani na nyota mwenzie wa muziki, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, alisema msanii anapotegemea kiki ili kutoka kimuziki ndio anaweza kuua kipaji chake na kupotea kabisa kwa kuwa maisha ya kiki ni mafupi hakuna mfano.

NYOTA wa Muziki wa kubembeleza Bongo, Jux amedai kukerwa na kiki za wasanii wenzake kwa madai zinamaliza vipaji vya nyota wanaofanya vizuri kwenye muziki.

Jux ambaye anashea vya ndani na nyota mwenzie wa muziki, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, alisema msanii anapotegemea kiki ili kutoka kimuziki ndio anaweza kuua kipaji chake na kupotea kabisa kwa kuwa maisha ya kiki ni mafupi hakuna mfano.

“Wasanii wengi hawafanyi vizuri kwa sasa maana wanategemea kubebwa na kiki ambazo zinawazidi ukubwa, yaani ni kama wanakimbia hadi wanapitiliza nyumbani kwao,” alisema Jux. Jux ambaye ni miongoni mwa wasanii wachache wenye mvuto kwa wanawake, alisema kutafuta kiki kunawalazimu wasanii kutoa nyimbo mpya kila baada ya muda mfupi kitendo ambacho kinasababisha nyimbo hizo kutokuwa na ladha wala mashiko.