Jokate aamua kuzama kwenye kikapu

MWANAMITINDO na mwigizaji  Jokate Mwegelo juzi Jumamosi aliteuliwa kuwa balozi wa mpira wa kikapu kwa vijana wanaochipukia na uzinduzi wa katika mchezo huo.

Joketi alisema kama atapata ushirikiano wa kutosha,  anaweza kuusogeza na kuufikisha mbali mchezo huu wa baisketi mbali na kuwapa fursa vijana ambao wanachipukia.

“Ninashukuru kwanza kupata nafasi ya kuwa balozi wa mchezo huu na ninaahidi kuwa nikipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadhamini wakubwa na Serikali naweza kuufikisha mchezo huu mbali zaidi,” alisema Joketi ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa katika fainali za mchezo  huo nchini Marekani.