Jada hana habari na wakwe

Jada Pinkett

Muktasari:

  • Akihojiwa katika Red Table Talk Jada alieleza kuwa siku zote amekuwa wazi kwa watoto wake na kuzungumza nao ili wafanye uamuzi sahihi sasa.

MWIGIZAJI Jada Pinkett amesema hafikirii kuingilia uhusiano ya watoto wake na haoni sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa anajitambua.

Akihojiwa katika Red Table Talk Jada alieleza kuwa siku zote amekuwa wazi kwa watoto wake na kuzungumza nao ili wafanye uamuzi sahihi sasa.

Kwa sababu hiyo haoni umuhimu wa kuwaingilia kwenye uhusiano wao kwa kuwa anaamini wanawachagua watu wanaowaona ni sahihi kwao.

Jada ambaye ni mama wa watoto wawili Jaden (19) na Willow (17) alisema amekuwa akiwapa uhuru ambao kwa kiasi kikubwa unawafanya kutambua na kutofautisha kati ya mema na mabaya katika jamii inayowazunguka.