Idriss mdogo mdogo huyooo

Tuesday October 10 2017

 

MSHINDI wa Big Brother-Hotshots 2014 aliye pia mchekeshaji na mwigizaji wa filamu nchini, Idris Sultan, amelamba shavu baada ya kuchaguliwa kuigiza filamu ya ‘The Blue Mauritius’.

Filamu hiyo itaandaliwa kwa ushirikiano na kampuni za D Street Pictures na Benoraya Pictures na wamemchukua Idris sambamba na Mtanzania mwingine, Ernest Napolean, huku bajeti yake ikitajwa kiasi cha Sh35 bilioni.

Kwa mujibu ya watayarishaji wa filamu hiyo itakayoanza kurekodiwa Machi mwakani, kazi hiyo itafanyikia katika miji ya Cape Town (Afrika Kusini), Berlin (Ujerumani), London (Uingereza), Paris (Ufaransa) na Acapulco (Mexico).

Idris alisema kuteuliwa kwake kushiriki filamu hiyo ni heshima na kwake na Tanzania pia.

“Ni fursa kubwa, kazi nzuri ya Kiumeni imetubeba mimi na prodyuza wangu, naahidi

sintawaangusha nitaigiza kwa kiwango cha juu,” alisema.