Ibrah tuzo moja, anachoonga!

Friday July 21 2017

 

MUIGIZAJI Bora wa kiume katika Tamasha la Filamu la Zanzibar, (ZIFF), Ibrahim Osward ‘Ibrah’ ameanza kuchonga baada ya kunyakua tuzo hiyo akidai kuna nyingine zinakuja kwa umri na kipaji alichonacho.

“Namshukuru Mungu kwa kuniweka juu na kushinda tuzo kubwa ya ZIFF. Naamini nitawakimbiza sana waigizaji wa kiume kwani umri wangu unaruhusu,” alisema Ibrah.

Kinara huyo wa filamu ya Tunu, alisema kwa kipaji alichonacho na kiu ya maendeleo aliyonayo anaamini ndoto zitatimia sio kwa kutwaa tuzo za ndani tu bali mpaka zile za kimataifa.

Umaarufu wa Ibra ulichangiwa zaidi na umahiri aliouonyesha kuputia filamu kadhaa ikiwamo Popo na tamthilia ya Siri ya Mtungi.