Hamisa ana nyodo huyo

Muktasari:

“Kuna wakati wa kuanza na huu ndiyo wakati wangu. Kuna wasanii wa kike wapo katika fani hii kitambo lakini wameigiza filamu nyingi hapa Dar es Salaam tu hivyo mimi kuanza tu kwa kuigiza filamu Afrika Kusini ni hatua,” alisema Hamisa.

MREMBO na mwanamitindo, Hamisa Mobetto ‘Mama Abdul’ amesema kuwa ameingia katika fani ya uigizaji kwa nguvu kubwa sana na anaamini kuwa anaenda kuziba mapengo yaliyoachwa na wasanii wakongwe ambao kwa sasa hawaonekani.

“Kuna wakati wa kuanza na huu ndiyo wakati wangu. Kuna wasanii wa kike wapo katika fani hii kitambo lakini wameigiza filamu nyingi hapa Dar es Salaam tu hivyo mimi kuanza tu kwa kuigiza filamu Afrika Kusini ni hatua,” alisema Hamisa.

Hamisa ameshiriki katika filamu ya Zero Player ambayo sehemu kubwa imerekodiwa Afrika Kusini na Tanzania. Filamu hiyo ilizinduliwa Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa sinema Cineplex cinema jijini Dar es Salaam.