Hamisa Mobetto amcharukia Idris

Muktasari:

Baadaye Idris aliamua kufuta picha hiyo na kisha kuandika ujumbe mwingine na kuomba radhi kutokana na tukio hilo huku akisema kuwa anawaheshimu wanawake wote na si kama watu wanavyofikiria.

Dar es Salaam. Baada ya Idris kuandika ujumbe wa utani kwa Diamond Platnumz katika siku yake ya kuzaliwa, Hamisa Mobetto alishindwa kuvumilia ndipo alimjia juu Idris Sultan.
Baadaye Idris aliamua kufuta picha hiyo na kisha kuandika ujumbe mwingine na kuomba radhi kutokana na tukio hilo huku akisema kuwa anawaheshimu wanawake wote na si kama watu wanavyofikiria.
“Heshima niliyonayo kwa wanawake na mama wote ni kubwa sana hasa hasa kwakua nimelelewa na mama mwenye uvumilivu, mpiganaji na wa kuijua dini sana. Jazba na huzuni wanazopitia wazazi ni kubwa sana hasa unapokaa na mtoto miezi 9 bila kuwa na uwezo wa kumshusha hata mara moja upumzike kidogo. Unavimba miguu, unalia sana, unapata vichomi, unabadilika sura, unashindwa hata kutembea na unaanza kula vitu huelewi. Mwaka baada ya mtoto kuzaliwa kuna mengi katika kumfunza kutembea kwa kushika meza, kutaja vimaneno vichache na kula vyakula vigumu pia kutambua zuri na baya kwa kuona. As for that najua hakuna thamani ya kipesa inayoweza kuwekwa kutathmini yote anayopitia mama. With this I respect women to the extent that thamani wanayoweza kulipwa nayo ni kwa maisha au kumpa mama moyo wako kabisa. This is the deep truth, the rest tunafanya utani because we just want to make things easy and laugh. My apologies if I have offended any women for this.
Regards,
Idris,” aliandika.