Hamisa Mobetto afunika hadi Sauzi

Friday November 10 2017

 

By RHOBI CHACHA

KWELI wa mbili havai moja, mwanamitindo na video queen matata, Hamisa Mobetto amezidi kung’ara baada ya kutwaa tuzo ya Starqt Awards katika

msimu wake wa nne.

Mrembo huyo alishinda tuzo hiyo kupitia kipengele  cha ‘People Choice Awards’, huku kile cha Super Mum, akishindwa kufurukuta mbele ya wenzake.

Mobetto alishinda tuzo hiyo akiiwakilisha vema Tanzania na Afrika Mashariki katika hafla zilizofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa wiki hii.

Tuzo hizo za Starqt zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine na hafla ya utoaji wa tuzo hizo kwa washindi zilifanyika Novemba 4, kwenye

Ukumbi wa Bedford View City, mjini Johannesburg.