Gabo ashtushwa na mavazi mjini

Tuesday June 12 2018

 

GABO Zigamba amefichua anaduwazwa na mabadiliko ya mavazi kwa vijana wa kileo, akidai yamewafanya wengi wao kuwa kituko badala ya kupendeza kama inavyofikiriwa.

Mwingizaji huyo mkali nchini, alisema ukiwa mjini na ghafla akitokea kijana unakutana na mavazi yake yanayokuduwaza kama si mavazi basi muonekano wa nywele zake au kujichora mwilini na kuwa kama kituko.

“Si kila jambo lina tija katika dunia hii, lakini siku hizi tunaishi katika ulimwenguni wa mikasa zamani mtu ukivaa suruali iliyochanika ilikuwa umaskini lakini kwa sasa ni fasheni, hii inanishangaza na kuonyesha mambo yamebadilika mno,” Gabo.

Gabo alisema kibaya zaidi kwa sasa mavazi yamekuwa ya muingiliano kati ya vijana na wasichana na kudai kuna haja jamii kuamka na kulinda maadili kwa vitendo, pia kujitahidi kujenga utamaduni wa kutumia lugha sahihi ya Kiswahili kwani ndio mtaji pekee utakaolinda Taifa hili.