Ferooz mambo hayako sawa

Muktasari:

  • Ferooz ameeleza sababu ya kutaka kufikia uamuzi huo ni kuonekana si kitu wakati ameutoa mbali muziki huo.

MKALI wa Bongofleva, Ferooz amesema, kuna wakati anatamani kuacha muziki lakini anashindwa.

Ferooz ameeleza sababu ya kutaka kufikia uamuzi huo ni kuonekana si kitu wakati ameutoa mbali muziki huo.

“Kikubwa kinachoniumiza nikiangalia game nilipolitoa mpaka lilipofika halafu bado naonekana ndio mkosefu namba moja.

“Kwa kifupi game linanisahau, mpaka nafikia kusema ni-quit kufanya muziki, ni-quit kufanya game, nitangaze nimeacha muziki. Nataka niache muziki lakini najikuta nashindwa kwa sababu umeshakuwa kwenye damu,” alisema Ferooz.

Ferooz aliyewahi kutamba na Kundi la Daz Nundaz na kufanya muziki kwa takribani miaka 20, amekuwa pia akifanya mambo mengine na kuachana na muziki huo.

Licha ya kukaa nje kwa muda mara kadhaa anajikuta akirudi. Mfano hivi karibuni alitoa ‘single’ ya‘Najaribu.’