Aubameyang alimsha dude Dortmund

Muktasari:

Mgaboni huyo ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika klabu hiyo

Munich, Ujerumani. Mshambuliaji wa Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ameachwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Wolfsburg kutokana na sababu za makosa ya kinidhamu.

Miamba hiyo ya Ujerumani imethibisha kuwa watareja baada ya mapumziko ya majira ya baridi bila ya mshambuliaji wake kinara wa ufungaji.

Aubameyang amefunga mabao 21, katika mechi 23 alizocheza msimu huu, lakini hatma yake ndani ya timu hiyo imekuwa shakani.

Mshambuliaji huyo amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Liverpool na Arsenal, pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa kutimkia China.

Adhabu hiyo mpya ni wazi itachochea lengo lake la kutaka kuachana na klabu hiyo.

Taarifa zinasema uamuzi huo umechukuliwa baada ya Aubameyang kushindwa kutokea katika kikao cha timu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon (28), alikosa mechi dhidi ya Stuttgart mwezi Novemba mwaka jana kwa sababu kama hizo na kumfanya kuondolewa katika kikosi kilichokwenda Milan.