Dogo Janja utamponza Young Dee akamatwe

Muktasari:

Mwandishi aliongea na Dogo Janja  na kusema hawezi kumjibu msanii huyo kwani hajui pia kama atakuwa anamjibu mtu mwenye akili timamu au tayari amekula unga.

BAADA ya Young Dee kusema kuwa yeye sio wa kufananishwa na Dogo Janja na Young Killer na kutaka waandishi wote wasimfananishe na wasanii hao, Dogo Janja amekuja juu kwa kujibu kauli hiyo huku akisema hawezi kubishana na mtu anayetumia unga.
Mwandishi aliongea na Dogo Janja  na kusema hawezi kumjibu msanii huyo kwani hajui pia kama atakuwa anamjibu mtu mwenye akili timamu au tayari amekula unga.
Akaongeza kuwa Young Dee kuomba asifananishwe na msanii kama yeye ni sawa kwani hata yeye hataweza kukubali kufananishwa au kukaa na mtu anaetumia dawa za kulevya kitu kinachomfanya awe anazungumza vitu vya ajabu.
"Young Dee ni Mteja, na hawezi kufanana na mimi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee. Akiacha Unga ndio ninaweza kuzungumza!