Dk Cheni yupo kiroho safi

Tuesday March 13 2018

 

WAKATI waigizaji wenzake wakongwe wakipambana na hali yao, Mahsein Awadh a.k.a Dk Cheni amefunguka kwa kudai yupo kiroho safi kutokana na tasnia hiyo kumfanyia mambo makubwa asiyoyatarajia.

Dk Cheni alisema wasanii nao wana nafasi na serikali inawakubali na kuwaweka katika kumbukumbu zao kitu cha kufurahia na kushukuru kwani naye ana mtaa uliopewa jina lake, yaani Mtaa wa Dk. Cheni maeneo ya Ilala jirani na Malapa.

“Nashukuru sana kwani si jambo dogo mtaa kuitwa jina lako tena la usanii kwa kweli nimefurahi na kama si kuwa muigizaji mkongwe au mwenye kuonekana na kukubalika ingekuwa ndoto tu jina langu kuitwa katika mtaa,” alisema Cheni.

Mwigizaji huyo alisema anaona ni fahari kubwa na heshima kwake na kwa wasanii wenzake kwani historia mara nyingi majina ya mitaa hutokana na sehemu husika au kwa watu maarufu tena wale wanasiasa kwake ni tukio kubwa, pengine angefikiri jinsi ilivyowahi kuzua utata Victor Wanyama alivyopewa Mtaa maeneo ya Ubungo.