Diana buana, hataki kulazimisha umaarufu

Muktasari:

Lakini mwigizaji Diana Kimaro, anayeigiza filamu na Elizabeth Michael ‘Lulu’, amefichua kuwa hapendi kuanika mambo yake hadharani, akikiri ni mtihani kwake.

MOJA ya changamoto  kubwa inayowakabili baadhi ya mastaa nchini ni kushindwa kuwa na mfumo unaoendana na nafasi zao, kisa umaarufu na kujikweza kupindukia.

Lakini mwigizaji Diana Kimaro, anayeigiza filamu na Elizabeth Michael ‘Lulu’, amefichua kuwa hapendi kuanika mambo yake hadharani, akikiri ni mtihani kwake.

“Sitaki kufanya ‘interview’ kwa sababu sitaki kulazimisha umaarufu, sipendi kuandikwa andikwa kwa sababu nipo bize na kazi zangu, hata sasa naongea na wewe kwa heshima tu,” alisema.

Alisema kwa sasa anaye Meneja anayemwongoza kufanya chochote ili kuendelea kumjengea heshima.