Beckham na mkewe waweka nguo zao sokoni

Saturday June 9 2018

 

WANANDOA mastaa David na Victoria Beckham wametangaza kuuza nguo zao walizovaa kwenye harusi ya mwana mfalme Prince Harry.

Lengo la kuuza nguo hizo si kurudisha gharama walizotumia, bali ni kutafuta fedha watakayoitoa kama msaada kwa wahanga wa shambulio lililotokea Manchester.

Kupitia harambee inayoendelea mtandaoni wanandoa hao wametangaza kuweka sokoni nguo hizo ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa wahanga hao.

“Nalilipenda gauni langu ila nawapenda zaidi binadamu wenzangu ndiyo sababu nipo radhi liuzwe ili kuwasaidia wenye uhitaji,”

Inadaiwa kuwa mavazi ya wanandoa hao yalikuwa ya thamani kubwana walikuwa miongoni mwa wageni waliotikisa kwenye harusi hiyo.