Angelina Jolie aja na filamu ya maisha yake

Muktasari:

Filamu hiyo ambayo imeongozwa na Angelina na pia akiwa kama Produza, imekuwa ni filamu ya kipekee ambayo imeongozwa na mtu kutoka Hollywood huku lugha ikitumiwa ya Cambodia ambapo ndipo stori ilipoakisiwa.

BAADA ya kuachana na mume wake ambaye waliweza kudumu kwa muda mrefu, Angelina Jolie amerudi kivingine kwa kuweza kuleta filamu inayofahamika kwa jina la First They Killed My Father ikiwa ni stori ya maisha ya kweli.
Filamu hiyo ambayo imeongozwa na Angelina na pia akiwa kama Produza, imekuwa ni filamu ya kipekee ambayo imeongozwa na mtu kutoka Hollywood huku lugha ikitumiwa ya Cambodia ambapo ndipo stori ilipoakisiwa.
Kwa mara ya kwanza kiliandikwa kitabu na mwanamama Loung Ung ambae katika miaka ya 1975 mpaka 80 katika vita iliyotokea huko Cambodia alishuhudia mambo mengi ya hatari ambapo wananchi wa Cambodia milioni moja walipoteza maisha.