VIDEO:Ali Kiba apewa mke ni mrembo acha!

Muktasari:

  • Kiba aliyekuwa ameandamana na ndugu yake, Abdu Kiba walifika katika Msikiti wa Ummul Kulthum wakiwa pamoja na rafiki yake wa karibu Gavana Hassan Joho.

HAIWI HAIWI imekuwa, asubuhi mapema harusi ya msanii Ali Kiba ilifanyika kwa shwange Mombasa nchini Kenya.

Kiba aliyekuwa ameandamana na ndugu yake, Abdu Kiba walifika katika Msikiti wa Ummul Kulthum wakiwa pamoja na rafiki yake wa karibu Gavana Hassan Joho.

Baada ya aya chache za korani kusomwa muda ukawadia na Sheikh Mohammed Kagera akashika kiganja cha Kiba na kumfungisha ndoa na mchumba wake Amina Khalef.

Na baada ya hapo, Kiba alisema maneno haya: “Mimi Ali Saleh nimekubali kumuoa Amina Khalef kwa mahari tuliyokubaliana na ikitokea sababu ya kuachana basi tuachane kwa wema.”

Tabasamu yake ya kawaida ikaja kinywani mwake baada ya kuitika mwito huo. Kiba alikuwa amevalia nguo inayotambulika kama Joho na kilemba na mkononi alikuwaameshika upanga kama ilivyo desturi ya tamaduni ya Uswahilini.

Baada ya kutoka msikitini waalikwa walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa ndugu yake Joho anayeitwa  Abu Joho eneo la hapo Kizingo.

Na baada ya harusi hiyo, mlo utakuwepo katika jumba la kifahari linalomilikiwa na Joho eneo la kaunti ya Kilifi.