Aisha Bui kaamua, sasa mtakoma

Tuesday June 12 2018

 

MWIGIZAJI wa kike wa filamu nchini, Aisha Bui amefunguka amejipanga ili kuhakikisha anaifanya kampuni yake ya kuzalisha filamu inakuwa ya kisasa kwa nia ya kukwepa usumbufu kutoka kwa baadhi ya watengenezaji wa kiume.

“Ukiangalia watayarishaji wa kike tupo wachache wengi ni wanaume labda ndio sababu ya usumbufu kwetu, hii inanifanya nijenge menejimenti ili kusaidia kufanya kazi vyema na kwenda na kasi ya dunia la filamu za kisasa,” alisema kimwana huyo.

Mwanadada huyo alisema inawezekana mara nyingi watoto wa kike wanachukuliwa kama pesa yao ni ya kupewa na wanaume hivyo kukosa uchungu nayo lakini kwake hategemei mwanamume katika kazi zake ni mtaji wake anatakiwa kuulinda ili usipotee kwani yeye si mmoja kati ya wale tegemezi.