Diamond bado anateswa na fumanizi la Ex wake

BAADA ya uzinduzi wa Chaneli ya Wasafi TV kwenye king’amuzi cha StarTimes kufanyika Jumatatu Juni 19, 2018 katika Hoteli ya Terrace pale Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam, Mwanaspoti lilifanya mahojiano magumu na mwanamuziki Diamond Plutnumz.

Mwanaspoti: Mambo vipi?

Diamond: Poa Mzima dada?

Mwanaspoti: Niko poa kabisa

Mwanaspoti: Ni kweli una stress kama alivyosema dada yako Esma?

Diamond: Hahaha, hapana bwana, labda stress kuhusu kuanzisha hii Wasafi Tv, ambayo nilikuwa najifikiria kwa muda mrefu na jinsi watu watakavyonipokea.

Mwanaspoti: Mapenzi yanakusumbua?

Diamond: Dah dada, haya maswali ndio siyataki kabisa, mimi nitaanzaje kusumbuliwa na mapenzi jamani.

Mwanaspoti: Hofu yako kubwa ni ipi?

Diamond: Kufa na kuwaacha watoto wangu.

Mwanaspoti: Mchezo upi wa utotoni unaukumbuka na kuupenda zaidi?

Diamond: Kibabababa

Mwanaspoti: Kitu gani unachojivunia tangu ulipopata umaarufu?

Diamond: Kupendwa.

Mwanaspoti: Chakula gani unakipendelea ?

Diamond: Wali.

Mwanaspoti: Ni wimbo upi hutaweza kuusahau?

Diamond: My Number One.

Mwanaspoti: Kitu gani kilichowahi kukutia aibu?

Diamond: Kumfumania mpenzi wangu wa zamani.

Mwanaspoti: Tangu umeanza kusafiri nje, nchi gani unaweza kuishi?

Diamond: Uingereza.

Mwanaspoti: Kama ukiwa Rais ni kitu gani cha kwanza kufanya?

Diamond: Kama nitakuwa Rais nitatengeneza mfumo ambao utatoa ajira kwa wengi.