Lulu Diva, Rich Mavoko wao kimya kimya

NYOTA kutoka lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz wana yao, kwani mahausiano yao ya kimapenzi wanapenda kuyafanya siri, lakini baadaye hutokea tu hadharani na kuwaumbua.

Nyota kutoka kwenye kundi hilo la bosi huyo wa Madale kama Harmonize na Romjs wamewahi kufanya mahusiano yao siri lakini mwishoe yakawa hadharani.

Hata bosi wao, Diamond naye alificha sana ishu yake na Hamisa lakini mimba ikamuumbua. Sasa unaambiwa nyota mwingine wa kundi hilo, Rich Mavoko pamoja na kuonekana mara kadhaa akiwa na mwanadada, Lulu Diva, ameendelea kukana kuwa wanakula vya kitandani pamoja.

Kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa Lulu DIva na Rich Mavoko ni wapenzi na hata tetesi hizo zimesapotiwa na picha zao mbalimbali ambazo zimekuwa zikionekana wakiwa pamoja kimahaba, lakini bado wamegoma kuthibitisha habari hizo, wanakataa.

Tetesi za wawili hawa kuwa pamoja zilianza tangu mwaka jana, baada ya kudaiwa Lulu Diva ametoswa na mpenzi wake na hata mahari yake aliyotolewa kurudishwa, baada ya kudaiwa kuchepuka na Mavoko. Hivi karibuni Lulu Diva ameachia kibao chake kipya akimshirikisha Mavoko, lakini kinachoendelea ni kutuma vipande vya wimbo huo katika peji zao za Instagram vikiashiria mapenzi. Je ni kweli? Tusubiri.