Masogange awakutanisha Kiba, Diamond

Muktasari:

  • Kuingia kwa Diamond kulibadilisha hali ya hewa uwanjani hapo badala ya kulia watu walishangilia, hasa baada ya  msanii huyo kumpa mkono Ali Kiba na pale alipopewa kipaza sauti aongee  

WASANII wa Bongo Freva, Ali Kiba na Naseeb Abdul 'Diamond' wamekutana na wamesalimiana kwa kupeana mikono katika shughuli ya kumuaga mpambaji wa video za Bongo Flava, Agnes Gerald ‘Masogange’  kwenye Viwanja vya Leaders Club.

Ali Kiba ndiye alikuwa wa kwanza kufika katika viwanja hivyo akiwa na gari yake aina ya BMW X5 na  kuwafanya maelfu ya watu waliokuwa uwanjani hapo walionyesha ishara ya mshangao, kwani ni siku tatu tu tangu afunge ndoa na mchumba wake Amina Khalef jijini Mombasa, lakini pia, mdogo wake, Abdul Kiba,  amefunga ndoa leo hii Jumapili jijini Dar es Salaam.

Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa amefika katika tukio hilo anajua kwamba dini yake hairuhusu lakini katika vitabu vya dini ya Kiislam vimeandika kwamba msiba ni moja ya ibada.

Mbali na Kiba, Diamond naye alingia akiwa na gari aina ya Prado na kwenda moja moja ilipo meza kuu na kuwasalimia wote.  Katika meza hiyo ndipo alipokuwa ameketi Ali Kiba na wageni wengine.

Kuingia kwa Diamond kulibadilisha hali ya hewa uwanjani hapo badala ya kulia watu walishangilia, hasa baada ya  msanii huyo kumpa mkono Ali Kiba na pale alipopewa kipaza sauti aongee