Tristan anaendelea kuisoma namba

Muktasari:

  • Inadaiwa kuwa licha ya wawili hao kushirikiana kwenye malezi ya mtoto Khloe anaonekana kuwa na hasira nae.

Licha ya kuwa hadi sasa Khloe hajazungumza chochote kuhusu kashfa ya usaliti inayomkabili mzazi mwenzie, Tristan Thompson bado hayuko sawa.

Inadaiwa kuwa licha ya wawili hao kushirikiana kwenye malezi ya mtoto Khloe anaonekana kuwa na hasira nae.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa muda so mrefu Khloe ataitikia wito wa ndugu zake wa kwenda Los Angeles.

Hata hivyo Tristan hatofikia kwenye nyumba hiyo ya familia hivyo atalazimika kutafuta makazi jirani hapo.

Wakati nyumbani kukifukuta mitandaoni nako hakujamuacha Tristan salama. Mashambulizi yanazidi watu wanaendelea kukomenti.

Watu wanamshambulia kwa kashfa hiyo na kulaumu kwa nini mtoto wao anaitwa True.

“Wanamuitaje mtoto True wakati baba yake ameshindwa kuwa mkweli na mwaminifu,” aliandika mtu mmoja.