Unaambiwa Pitt azidi kujiweka kwa Oxman

Muktasari:

  • Penzi kati ya wawili hawa linaonekana kukolea kila kukicha licha ya ratiba zao kuwabana na kusababisha wakati mwingine wasionane.

NI takribani miezi sita tangu uhusiano kati ya Brad Pitt na Neri Oxman uanze na wawili hawa wanaonekana kuwa moto wa kuotea mbali.

Penzi kati ya wawili hawa linaonekana kukolea kila kukicha licha ya ratiba zao kuwabana na kusababisha wakati mwingine wasionane.

Chanzo cha habari kimeliambia jarida la Us weekly kuwa wawili hao wamekuwa wakizungumza mara nyingi kwa simu kufidia muda wanaoshindwa kuonana.

Neri anaonekana kukwepa kumulikwa na kamera jambo ambao limekuwa likijitokeza mara kadhaa anapokuwa na nyota huyo.