‘Nilimblock Wema Sepetu’

Muktasari:

“Hela nzuri alafu mapenzi matamu na pia mapenzi mazuri yanahitaji hela kwahiyo ukianza kufikiria mapenzi mazuri lazima utafikiria kuhusu hela kwa hiyo nikifikiriaga kuhusu mapenzi na hela huwa inakuja sambamba kabisa,” alisema.

Dar es Salaam. IDRIS sultan amefunguka kuwa katika vitu anavyofikiria mara nyingi akiamka huwa anafikiria hela na mapenzi na kwake ndio vitu vya umuhimu zaidi kwanza kabla ya mengine kuanza kufikiria.
“Hela nzuri alafu mapenzi matamu na pia mapenzi mazuri yanahitaji hela kwahiyo ukianza kufikiria mapenzi mazuri lazima utafikiria kuhusu hela kwa hiyo nikifikiriaga kuhusu mapenzi na hela huwa inakuja sambamba kabisa,” alisema.
Pia aliongeza juu ya mahusiano yake na Wema ambapo alikana kuwa na uhusiano tena na mrembo huyo na kudai kuwa bado yupo ‘singo’.
“Mtu wa mwisho mimi kumblock kwanza kwenye Instagram yangu ni Wema, aliniuzi ila kwa sasa ni fresh,” aliongeza.