Wolper wala hajapoteza mjue!

Tuesday May 15 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

MWIGIZAJI wa kike wa filamu nchini, Jacqueline Wolper Massawe amesema alizaliwa mrembo na kuwa mmoja kati ya wanawake nyota wanaojua kulinda urembo wao, huku akisisitiza hajapoteza kitu kwa kutoka kwake kwenye umalkia hadi kuwa mtu maarufu.

“Nimekuja duniani nikiwa Queen mrembo nisiyechuja na ninafurahia kuwa staa wa Bongo Movie naamini kila nionekanapo kuna watu roho zinawalipuka, naulinda sana mwonekano wangu,” alisema Wolper.

Msanii huyo alisema kupata umaarufu inaweza kuwa rahisi, lakini kudumu kama mtu nyota ni ngumu kwani unahitaji sana kujilinda na mambo mengi zikiwemo kashfa mbalimbali.

Wolper alisema kuna wakati mtu anaweza kuzidiwa na mambo na kujutia akiujutia umaarufu wake.