Uigizaji wampa dili Nkwabi

Tuesday May 15 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

KINARA wa tamthiliya iliyowahi kufunika siku za nyuma ya 69 Records, Nkwabi Juma amesema kujitosa kwake kwenye uigizaji kumemrahisishia mambo na kupata dili

kadhaa za ulinzi katika matamasha mengi ndani na nje ya nchi.

“Naheshimu sanaa, kwani kwa sasa kila ikitokea shughuli yoyoye na kuitwa kwa ajili ya usalama mapatano yanakuwa rahisi kwani wengi wananifahamu kupitia filamu na tamthiliya nyingi nilizoigiza, kwa hili namshukuru Mungu,” alisema Nkwabi.

Nkwabi aliwashauri wenzake kujiwekezea kazi nyingine ili kutengeneza maslahi kwani yeye anawalinda watu maarufu na kusisitiza mchongo huo umetokana na ushiriki wake wa fani ya sanaa iliyompa umaarufu.