Tristan amfanyia kitu mbaya Khloe

Friday April 13 2018

 

TAARIFA za mpenzi wake kumsaliti huenda zikamfanya Khloe Kardashian ajifungue kabla ya muda, kufuatia dalili za uchungu zilizoanza kumtokea.

Mtandao wa TMZ juzi uliweka video iliyomwonyesha Tristan akiwa kimahaba na wanawake wawili na baadaye kuondoka na mmoja kwenda nae hotelini.

Picha hizo zilizonaswa kwenye kamera ya usalama zilipigwa Oktoba mwaka Jana wakati huo Khloe akiwa na ujauzito wa miezi mitatu.

Hii ina maana kuwa Tristan alikuwa na Wanawake wengine ilihali akiwa kwenye uhusiano na Khloe.

Binti huyo kutoka katika familia ya mastaa, amejikuta kwenye mkosi huo ikiwa umesalia mwenzi mmoja ajifungue.

Tayari familia imefunga safari kumfuata anakoishi huko Cleveland na imeonyeshwa kukerwa mno na kitendo hicho cha Tristan.

Mmoja wa wanawake walioonekana kwenye video hiyo ameiambia TMZ kuwa hakufahamu kama Khloe ni mjamzito.

Marie alisema baada ya kugundua kuwa Khloe na Tristan wana uhusiano siriazi aliamua kukata mawasiliano nae.