Nyie Shamsa, Chid ni chechee

Friday April 13 2018

 

By RHOBI CHACHA

CHEZEA ukwe wenza wewe, ni noma unaambiwa. Staa wa Bongo Movie, Shamsa Ford ameibuka na kudai ikitokea mumewe akataka kuongeza jiko basi ataomba talaka yake fasta kwani, hataki kushare kabisa. Shamsa amedai kuwa, hatua hiyo inatokana na wivu alionao kwa muemwe, Chid Mapenzi na kuwa tangu amefunga ndoa amekuwa akifurahia maisha.

Hata hivyo, Shamsha amekuwa akiporomosha vichambo vya maana huko kwenye mitandao ya kijamii, amefunguka kuwa hawezi kuishi mbali na Chid.

Lakini, Shamsa amelifungukia Jarida la Jiachie kuwa tangu ameingia kwenye ndoa miaka miwili iliyopita, huku akiendelea kuishi kwa raha mustarahe huku ndoa za mastaa wengine zikiishia njiani kwa dhoruba. “Nampenda sana Chid hivyo siwezi kuwa naye mbali na sasa tunajipanga kimaisha kabla ya kuanzisha familia. Tunatamani mtoto, lakini hatuwezi kukurupuka kwa hilo ila ndani ya mwaka huu tunaanza kutafuta mtoto na tunamuomba Mungu atusaidie,” alisema Shamsa.