Ne-Yo ammwagia mkewe sifa kibao

Friday April 13 2018

 

MWANAMUZIKI Neyo ameweka wazi kuwa tabia zake za sasa zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mkewe Crystal Smith.

Nyota huyo ameeleza kuwa mkewe ndiye amemfanya kuwa Mwanaume bora kwani hapo awali hakuwa kama alivyo sasa.

Amedai kuwa kwa mara ya kwanza alipokutana na mwanamke huyo aliona wazi kuna vitu anatakiwa kubadilika na ndivyo ilivyokuwa.

“Nilivyo sasa ni kazi ya Crystal kila kukicha hachoki kunifundisha mambo mazuri, ni mwanamke jasiri, mwenye upendo na huruma na anayejitambua yeye ni nani,”

Amesema hata wimbo wake mpya ‘Good man’ ameimba ukweli wa maisha yake na kuelezea mchango wa mkewe kwake.