Msikie Thea kuhusu michepuko

NYOTA wa Filamu Bongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amewasihi wanawake hasa wale nyota kuachana na mahusiano ya kutoka na wanaume wa watu kwani mara nyingi mapenzi yao yamejaa shaka na hofu huku pia kukiwa hakuna mipango endelevu.

“Ukiwa na mwanamume asiye wako, mtu mwenye familia yake, hakuna mahusiano ya kweli bali ni kupoteza muda kwani unaweza kuachwa popote hata nauli bodaboda usiachiwe, na kesho utaambiwa ‘wife’ alitokea,” alisema Thea.

Thea anasema kuwa mwanamke akiwa na mchepuko hata siku akidanganywa si rahisi kutambua kwani mwanamume anaweza akapata hata mwanamke mwingine lakini akimweleza mke wake yupo hawezi kutoka si rahisi kubaini ukweli.