Mjeshi ana siri nzito moyoni

Muktasari:

Mjeshi ambaye ni mchekeshaji mwenza na Ebitoke alisema kipengele hicho kimekuwa sehemu kubwa ya historia kwake na hataweza kukisahau kamwe.

MCHEKESHAJI anayekuja kwa kasi Bongo, Hassan Daffur ‘Mjeshi’ amedai hatosahau jinsi alivyopata shida wakati akiigiza katika filamu ya Sema kama kijana wa kihuni aliyekuwa hana sehemu ya kulala na mvuta bangi.

Mjeshi ambaye ni mchekeshaji mwenza na Ebitoke alisema kipengele hicho kimekuwa sehemu kubwa ya historia kwake na hataweza kukisahau kamwe.

“Filamu ya Sema ilikuwa inahitaji uhalisia. Wakati nikiwa narekodi na kuvuta hisia kama mhuni nilizidiwa na kujikuta kama nimezingirwa na majini kweli nao wakitaka kuvuta Bangi,” alisema Mjeshi.

Mjeshi alisema tangu aanze kuigiza hiyo ndio ilikuwa sehemu ngumu kwani alitamani apige kelele kama mtu aliyepagawa. Hata hivyo alisema anachofurahia ni kuweza kuigiza katika kiwango cha juu zaidi na kung’ara na kumfunika Ebitoke.