Kumbe sio kila mtu ni mchekeshaji

Tuesday May 15 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

MAULID Ali ‘Maufundi’, mchekeshaji wa Komedi Bongo amefunguka kwa kudai sio kila mtu ana kipaji cha kuchekesha kwa sababu fani hiyo ni ngumu inayohitaji ukomavu ili kumudu kuwavunja mbavu watu walionuna.

“Kulingana na hali ya soko kwa sasa filamu, kazi hailipi kwa vile Filamu za Kizungu zimejaa tela kila kona. Pia, ilitakiwa filamu zetu tuigize katika majukwaa, lakini kuchekesha watu si mchezo unaweza kuona watu wanacheka kumbe wanakucheka,” alisema Maufundi.

Maufundi alisema hiyo ndio sababu inayowakosesha wachekeshaji wa Kitanzania kuchekesha jukwaani (Stand up Comedy). Pia, hata utamaduni wa Watanzania kuingia kwa ajili ya maonyesho ya moja kwa moja jukwaani tofauti na siku za nyuma.