Jay Z ampaisha Nyong'o kiaina

Saturday July 1 2017

 

HUKU staa mwigizaji Lupita Nyong’o akiwa kwenye pilka pilka za uandaaji wa filamu yake  ijayo‘Black panther’ itakayotoka mwakani, rapa mkali Jay Z kamchukua na kumtumia kupromoti ujio wa albamu yake mpya iliyotoka saa chache zilizopita (usiku wa kuamkia  leo Jumamosi)Jay Z ambaye amekuwa akijitahidi sana kuwa mbunifu kwenye miradi yake ya siku hizi, kamtumia Lupita kuigiza kwenye Teasre ya albamu hiyo ya 4.44 iliyotoka kupitia tuvuti yake ya kupakia na kupakua  muziki Tidal.

Kwenye teaser hiyo ya sekunde, Lupita anaonekana akiwa amepiga magoti huku akitiririkwa na machozi ishara ya mtu anayepitia maumivu makali ya unyanyasaji kabla ya kukatika.

Kazi za hivi karibuni za Jay Z zimekuwa zikiwahusu sana watu wenye asili nyeusi na huenda ndio sababu moja ya kumtumia Lupita ambaye amekuwa maarufu sana duniani kutokana na ujasiri wake wa kuigizaji na kuusifia mwonekano wake dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kando na kuwa teaser ya kiki yua albamu yake, 4.44 inasemekana kwamba pia itatoka kama filamu fupi.